Mchanganyiko wa dawa za Ibuprofen na Codeine unavyohatarisha maisha

M

Shirika la Ulaya la madawa la Ulaya (EMA) limetoa tahadhari wiki hii kuhusu athari za utumiaji wa mchanganyiko huu, ambao hutengenezwa kwenye maabala kwa muundo wa tembe au chembechembe zinazochanganywa na maji na katika baadhi ya nchi katika bara hilo huuzwa katika maduka ya dawa bila idhini ya daktari.

Kamati ya tathmini ya shirika la madawa la Ulaya iliashauri kuwa kijikaratasi kinachowekwa ndani ya paketi ya dawwa hizi kinajumuisha onyo kuhusu “smadhara mabaya, mkiwemo kifo, hususan wakati dawa hizi zinapotumiwa kwa kipindi kirefu zaidi kwa dozi ya juu zaidi kuliko iliyoshauriwa.”

“Kamati hiyo ilitathmini visa kadhaa vya figo, utumbo na mfumo wa utaji uchafu ambavyo vimeripotiwa kuhusiana na matumizi mabaya ya codeine na uraibu wa mchanganyiko wa ibufen ambavyo vimesababisha vifo,” iliongeza.

Ibuprofen ni mojawapo ya madawa ya kudhibiti maumivu yanayotumiwa zaodi katika kudhibiti maumivu yanayosababishwa na vidonda mwilini kote duniani.

Ni sehemu ya lundi la madawa linalofahamika kama nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs) pamoja na aspirin, ketoprofen, na naproxen, miongoni mwa madawa mengine, na hufanya kazi mwilini kwa kupunguza homoni ambazo zinasababisha maumivu na uvimbe.

Codeine iko katika kundi la opioid , sawa na dawa ya morphine au oxycodone. Wakati inapoingia mwilini, sehemu ndogo ya dawa hiyo hubadilika na kuingia mwilini, na kuingia kwenye mfumo wa neva na kubadili jinsi ubongo unavyotambua maumivu ya mwili na kuzuia maumivu.

Hutumika kutibu maumivu makali wakati dawa kama acetaminophen, aspirin, au ibuprofen pekee hazitoshi kuzuia maumivu, na kupunguza kikohozi wakati dawa nyingine zimeshindwa kufanya kazi.

Pia hupunguza msongo wa mawazo na wasiwasi unaosababishwa na maumivu.

“Kihistoria imekuwa ikitumiwa katika kipindi cha baada ya upasuaji mdogo. Kama uvimbe umetolewa kooni unaweza kupewa codeine kwa siku chache,” Peter Chai, daktari wa tiba ya dharura, na mhadhiri katika chuo kikuu cha Havard aliielezea BBC Mundo.

Chai alifafanua kuwa nchini Marekani codeinehuchanganywa na paracetamol badala ya ibuprofen, lakini kwa njia hii haitumiwi ipasavyo na hivyo kutoifanya isiingilie mfumo wa neva na ubongo. Utendaji wa Codeine katika mwili wa mtu na mtu ni tofauti “katika njia tofauti na kwa kasi tofauti’’ .

Hasara nyingine kubwa ya codeine ni kwamba husababisha uraibu wake kwa mtumiaji, kwahivyo matumizi yake hayashauriwi kwa zaidi ya siku tatu.

“Kuna mambo ma mawili ya kuangalia katika mchanganyiko wa tembe ya codeine na ibuprofen. Kuna uwezekano wa matumizi mabaya ya codeine kwasababu ya kuwa katika kundi sawa na la morphine, kama vile oxycodone, kama hydromorphone,” Chai said.

“Lakini kama mtu fulani haitumii ipasavyo au anaitegemea pekee pamoja na ibuprofen kama dawa ya kutuliza maumivu, hapo ndio anajipata katika matatizo kwasbabu zinafahamika kama sumu zinazohusiana na kuharibika kwa utumbo na figo,” aliongeza.

EMA ilisema katika taarifa yake kwamba wakati dawah ii inapotumiwa kwa dozi ya viwango vya juu kuliko ile iliyoshauriwa au kwa muda mrefu, inaweza kusababisha kile kinachoitwa renal tubular acidosis, ikimaanisha kuharibika kwa mafigo kwa kuyazuia kuondoa asidi kutoka ndani yad amu kwa njia ya mkono.

Kutofanya kazi kwa mafigo kunaweza kusababisha viwango vya juu zaidi vya potassium katika damu, na hivyo kusababisha kudhoofika kwa misuli na kizunguzungu.

Kwa watu wazima ambao tayari wana matatizo ya kiafya ya figo na shinizo la damu , Ibuprofen pia inaweza kusababisha uharibifu wa figo kwasababu husababisha kupungua kwa mtiririko wa damu katika eneo hilo, anasema dokta Chai.

“Kumekuwa na msukumo wa kutaka mchanganyiko wa dawa hizi ziondolewe kwenye soko kwasbabu zinaleta matatizo ya kiafya kwa wale wanaozitumia ,” alisema mtaalamu huyo ambaye ni profesa katika Chuo kikuu cha Harvard.

EMA ilisema kuwa wagonjwa wanapaswa kuomba ushauri kwa madaktari wao iwapo wanataka kutumia codeine na ibuprofen kwa muda zaidi ya ule waliopangiwa na daktari au kwa dozi ya juu zaidi kuliko iliyoshauriwa.

Kutofanya kazi kwa mafigo kunaweza kusababisha viwango vya juu zaidi vya potassium katika damu, na hivyo kusababisha kudhoofika kwa misuli na kizunguzungu.

Kwa watu wazima ambao tayari wana matatizo ya kiafya ya figo na shinizo la damu , Ibuprofen pia inaweza kusababisha uharibifu wa figo kwasababu husababisha kupungua kwa mtiririko wa damu katika eneo hilo, anasema dokta Chai.

“Kumekuwa na msukumo wa kutaka mchanganyiko wa dawa hizi ziondolewe kwenye soko kwasbabu zinaleta matatizo ya kiafya kwa wale wanaozitumia ,” alisema mtaalamu huyo ambaye ni profesa katika Chuo kikuu cha Harvard.

EMA ilisema kuwa wagonjwa wanapaswa kuomba ushauri kwa madaktari wao iwapo wanataka kutumia codeine na ibuprofen kwa muda zaidi ya ule waliopangiwa na daktari au kwa dozi ya juu zaidi kuliko iliyoshauriwa.

About the author

Olivia Wilson
By Olivia Wilson

Categories

Get in touch

Content and images available on this website is supplied by contributors. As such we do not hold or accept liability for the content, views or references used. For any complaints please contact adelinedarrow@gmail.com. Use of this website signifies your agreement to our terms of use. We do our best to ensure that all information on the Website is accurate. If you find any inaccurate information on the Website please us know by sending an email to adelinedarrow@gmail.com and we will correct it, where we agree, as soon as practicable. We do not accept liability for any user-generated or user submitted content – if there are any copyright violations please notify us at adelinedarrow@gmail.com – any media used will be removed providing proof of content ownership can be provided. For any DMCA requests under the digital millennium copyright act
Please contact: adelinedarrow@gmail.com with the subject DMCA Request.